Maisha yako pamoja na Mungu

April 20, 2018

"Kiwango cha heshima yako kwa mtu hutokana na kwa kiasi gani unavyomjua Mungu" Mchungaji Thadey Lukuwi.
INyakati 28:9 imeandikwa "Nawe Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu na kwa nia ya kumkubali, kwa kuwa Bwana hutafutatafuta mioyo yote ya fikira; ukimtafuta atao ekana nawe,  UKIMUACHA ATAKUTUPA MILELE"
Heshima yako kwa Mungu huongezeka kwa vile utakavyozidi kuwa na hamu ya kumjua Mungu/kujifunza neno la Mungu na kumtumikia kwa ukamilifu.
Ukimjua vizuri Mungu wako, utakuwa na mawazo mazuri kwake., kwa maana nyingi utajiweka wakfu kwake kwa mali zako , mwili wako na kwa roho yako pia.
SWALI:  Unawezaje kumtii Mungu husiyemjua vizuri?
Husipomjua Mungu vizuri hutaweza kumtimikia kwa kiasi cha utimilifu. Mtumikie Mungu kwa kuzipenda na kufurahia huduma, uwe na ari ya kutamani kufanya jambo kwa ajili ya Mungu.

No comments:

Powered by Blogger.